Mwamuzi Jonesia Rukyaa (28) kuwa ndiye atakayezihukumu Yanga na Simba
Mwandishi Wetu, Dar es SalaamSIMBA na Yanga, Jumamosi hii zinashuka uwanjani kuwania pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, jana Jumanne Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimtangaza Jonesia Rukyaa kuwa ndiye atakayezihukumu timu hizo mbili katika mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Rukyaa mwenye umri wa miaka 28, atashuka uwanjani akiwa na kumbukumbu ya kuzichezesha timu hizo kongwe kabisa hapa nchini katika mechi tatu za ligi kuu na moja ikizikutanisha zenyewe katika mchezo wa kirafiki wa Nani Mtani Jembe.
Yanga aliichezesha katika mechi moja kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Mbeya City msimu huu, nayo ilishinda kwa mabao 3-0.
Hata hivyo, mechi hiyo ya Jumamosi hii baina ya wapinzani hao itakuwa ni ya pili kwake kuzichezesha Simba na Yanga baada ya ile ya Mtani Jembe ambayo aliwahi kukiri kuwa alikumbana na changamoto nyingi kutokana na ukubwa mechi hiyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.