Wednesday, January 13, 2016

Anonymous

MAGUFULI Siku 70 Ikulu, Safari Mbili? Maamuzi Z’bar? Ujambazi Dar? Ufisadi na CHADEMA?

Dar sio salama, matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yatishia maisha ya wengi… Jecha wa Tume ya Uchaguzi ZEC atoka mafichoni, aibukia sherehe za Mapinduzi, bango la ubaguzi laleta kizaazaa Zanzibar, Mbunge Tundu Lissu asema ajenda ya kupambana na ufisadi ni ya kudumu CHADEMA. 

Rais Magufuli aombwa kuingilia kati kumaliza mgogoro wa Zanzibar baada ya mazungumzo ya viongozi wa visiwani humo kuonekana kutozaa matunda, Dk. Shein amesema uchaguzi Zanzibar utarudiwa, inasubiriwa tarehe… Wasomi wakosoa Mawaziri kutimua watumishi mbalimbali, mtoto wa miaka 13 afungishwa ndoa ya kimila Shinyanga. 

Waziri wa Biashara Charles Mwijage amesema watengenezaji wa Chibuku waboreshe kinywaji hicho ili wasio na uwezo watumie kinywaji hicho. 

Rais Magufuli kiboko, atoka nje ya Dar mara mbili na kupanda ndege mara moja tu ndani ya siku 70… Hii ni sehemu ya uchambuzi wa Magazeti ya leo, unaweza kusoma magazeti kwenye link hii mtu wangu >>> MAGAZETI

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.