WATU
wawili wamefariki dunia Papo hapo baada ya Gari walilokuwa wakisafiria
lililobeba Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kwenda
mkoani mkoani Mbeya kupata ajali Eneo la Kitonga Wilaya ya Kilolo mkoani
Iringa.
Ajali
hiyo imetokea leo alfajiri baada ya dereva wa Gari hilo kujinusuru
kugongana uso kwa uso na gari jingine, hivyo kulazimika kuingia nyuma ya
lori na kupelekea vifo vyao.
Kwa
mujibu wa Wakala Afisa mauzo wa magazeti ya Mwananchi Mkoa wa Iringa
Alex Kadea ambae alifika Eneo la tukio ameithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa kandiliyetu na kuwa waliofariki dunia wote wawili walikuwa ni madereva wa Gari hilo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.