Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
MACHOZI ya furaha! Sekunde chache baada ya Mahakama ya Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Morogoro kumuachia huru Katibu wa Taasisi na
Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, mashehe kadhaa na
wanawake waumini wa Kiislamu waliofurika eneo hilo, waliangua vilio
wakiwa hawaamini kilichotokea mbele yao.
Shehe Ponda, aliyekuwa mahabusu kwa kesi ya uchochezi zaidi ya miaka
miwili, akituhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali katika Viwanja vya
Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, aliachiwa huru
Jumatatu ya wiki hii.
Mara baada ya Hakimu Mary Moyo kutoa uamuzi huo, kundi la mashehe na
wanawake kutoka Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro waliangua vilio baada
ya kumuona kiongozi wao huyo akitoka katika geti la mahakama hiyo akiwa
huru.
“Nafurahi kuwa huru baada ya kuwa nimesota rumande kwa zaidi ya miaka
miwili baada ya kukosa haki yangu ya msingi ya dhamana, kwenye kesi hii
yenye dhamana ambayo kwa sababu ambazo zisijui, DPP alifunga dhamana
yangu, nashukuru kuwa huru na mengi tutazungumza baadaye, ” alisema
Shehe Ponda huku akiwa na furaha.
Baada
ya kutoka mahakamni hapo, shehe huyo na kundi la waumini walielekea
kwenye Msikiti wa Dini Moja Mungu Mmoja uliopo maeneo ya Kiwanja cha
Ndege mkoani hapa kwa ajili ya
Note: Only a member of this blog may post a comment.