Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.
Kutokana na kasi ya Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli hasa katika kupunguza matumizi ya
serikali, watu wengi kutoka kona mbalimbali za Bara la Afrika
wameonekana kumkubali kwa kutengeneza ‘Hashtag’ katika mtandao wa
Twitter ya #WhatWouldMagufuliDo wakimaanisha kama angekuwa Magufuli angefanyaje.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Rais Magufuli kufuta sherehe za Uhuru na badala yake wananchi kuitumia siku hiyo kushiriki katika zoezi la kusafisha mazingira ili kupambana na ugonjwa wa kipundupindu nchini.
Rais Magufuli pia alipunguza bajeti ya hafla ya wabunge katika siku ya uzinduzi wa Bunge kutoka milioni 225 mpaka milioni 24 na kuamuru fedha zilizobaki zipelekwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda.
Matumizi mengine aliyoyapunguza Rais Magufuli ni pamoja na kusitisha ziara za nje kwa viongozi wa serikali na kuzuia bajeti ya serikali kutumika katika kuandaa kadi za Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya na badala yake fedha hizo zisaidie kulipa madeni ya serikali.
Punguzo lingine alilolifanya Rais Magufuli ni la kufuta maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani na badala yake fedha za maadhimisho hayo zitumike kununua dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs).
Tangu Rais Magufuli aapishwe Novemba 9, 2015 zifuatazo ni baadhi ya meseji zinazosambaa katika mtandao wa Twitter zikionyesha kumkubali utendaji kazi wake wa kupunguza matumizi.
When she wants some silverware jewelry but then you’re smart so you start thinking: #WhatWouldMagufuliDo pic.twitter.com/etvFZy9iPx
— Given Edward (@GIVENALITY) November 26, 2015
My girlfriend wanted money for eye-liner, I asked myself #WhatWouldMagufuliDo ; we used office marker pens instead pic.twitter.com/mdQL7OdRFr — Dave (@MyUglyMustache) November 26, 2015
After my Iron stopped working before buying a new one i asked myself #WhatWouldMagufuliDo and Voila!! pic.twitter.com/v3PIhvAlOA
— Mahmud (@MahmudKullane) November 26, 2015
I wanted to buy a cap but the I thought of #WhatWouldMagufuliDo pic.twitter.com/wIlsCqW7fx — Victor Mochere (@VictorMochere) November 26, 2015
I seriously wanted to increase Uganda’s defence budget but then tweeps asked me #WhatWouldMagufuliDo and I was like pic.twitter.com/Z617mEJoCo
— Allan Ssenyonga (@ssojo81) November 26, 2015
Credit: www.theguardian.com
Note: Only a member of this blog may post a comment.