Wednesday, December 2, 2015

Anonymous

Huwezi Amini: Hivi Ndivyo Mtoto wa Miaka 9 Alivyonaswa Kaiba Gari Jijini Dar... (+Audio) #Hekaheka

Hii stori ukiisikiliza unaweza usiamini lakini ndio hivyo imetokea Dar, mama wa mtoto huyo amesema mwanae alikuwa mtundu sana tangu akiwa mdogo.. alifanya kila jitihada kumdhibiti lakini hakufanikiwa chochote !! 

Tukio likatokea siku chache zilizopita, mtoto huyo alikuwa maeneo ya viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam… jamaa mmoja aliacha funguo ya gari akawa anafanya mazoezi, mtoto huyo akaingia ndani ya gari na kuondoka nalo. 
Kilichofanya mtoto huyo akamatwe  ilikuwa hivi;
kwanza alimgonga dereva wa bodaboda, akamgonga mwanajeshi na mwanafunzi mmoja maeneo ya Kimara, baadae gari ikatoka tairi… watu wakamkamata na kumpeleka Polisi. 

Katika mahojiano aliyofanyiwa mtoto huyo amesema alikuwa akifundishwa na watu fulani kuendesha gari na lengo lao ilikuwa wamtume kuiba gari aina ya land cruiser.

Stori yote kwenye hekaheka hii hapa mama yake akisimulia tukio zima.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.