Wanajeshi wakijaribu kuingia katika Hoteli ya Radisson Blu mjini Bamako.
Wanajeshi wenye silaha nchini Mali wameingia katika hoteli ya
Radisson Blu mjini Bamako baada ya watu wenye silaha kuishambulia na
kuwashikilia watu mateka.
Baadhi ya wananchi wakiokolewa kutoka kwenye hoteli ya Radisson Blu.
Ripoti zinasema mateka 80 wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ambayo inamilikiwa na Wamarekani.Awali, kampuni inayomiliki hoteli hiyo ya Rezidor Hotel Group ilisema watu 170 walikuwa wameshikiliwa mateka na watu hao.
Baadhi ya ripoti zinasema watu walioshambulia hoteli hiyo yenye vyumba 190 huenda wakafika 10.
Note: Only a member of this blog may post a comment.