Barafu zikiwa zimetanda.
New Zealand
WATU saba wakiwemo watalii wa Kiingereza
wanne, raia wa Australia wawili pamoja na rubani wamefariki kwenye
ajali ya helikopta mapema leo nchini New Zealand.
Ajali hiyo imetokea baada ya helikopta hiyo yenye injini moja wakati
ikipaa angani, kuanguka kwenye bonde lililo na barafu katika huko South
Island eneo la Fox Glacier lililopo kwenye ufukwe wa Magharibi mwa nchi
ya New Zealand. Picha zilizopatikana zinaonesha helikopta hiyo ikiwa imenasa katikati ya miamba miwili mikubwa kwenye bonde hilo.
Mpaka sasa helikopta nne zimetumwa eneo
hilo kutafuta mabaki ya ndege na kutoa miili ya marehemu licha ya
changamoto zilizopo eneo hilo ikiwa ni pamoja na miamba mingi, barafu na
milima na mabonde hivyo kufanya vikosi vya uokoaji kushindwa kufika
kwenye eneo la tukio kirahisi
Ajali kama hiyo ilitokea mwaka 2010
wakati ndege iliyokuwa imebeba waruka mwavuli ilipoanguka baada ya kupaa
angani kutoka Fox Glacier na kuua watu tisa.
Note: Only a member of this blog may post a comment.