Mwili wa marehemu ukiwa umefunikwa baada ya kutokea kwa mauaji hayo.
Watu wenye silaha wamewapiga risasi na kuwauwa watu saba usiku wa
kuamkia leo katika mji mkuu wa Burundi- Bujumbura Watu hao waliokuwa
katika kilabu cha burudani mjini Bujumbura waliamrishwa walale chini
kabla ya kufyatuliwa risasi na kuuawa papo hapo.
Wakazi wa Bujumbura wakiyakimbia makazi yao kutokana na machafuko hayo.
Meya wa mji huo ametaja kisa hicho kama mauwaji ya kinyama.Waliwaua
watu 7 na kuwajeruhi wengine wawili alisema Freddy Mbonimpa meya wa mji
huo. Awali wenyeji wa vitongoji vya mji wa Bujumbura walionekana
wakitoroka makwao kwa hofu ya Mauaji hayo.Katika juma lilopita pekee , watu 20 wamekufa, hasa kwenye mitaa ambako upinzani una nguvu. Watu zaidi ya laki mbili wamekimbilia nchi za nje. Katika wimbi la machafuko ya kisiasa nchini humo, tangu mwezi Aprili, pale rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia ya kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu.
(Chanzo: BBC)

Note: Only a member of this blog may post a comment.