KIAPO! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji
matata Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Cookie’ kufunguka kuwa kamwe
hatajihusisha kwenye ishu yoyote ya sherehe inayomuhusu staa mwenzake
Wema Sepetu ‘Madam’ isipokuwa kwenye tatizo la msiba unaomuhusu.
Wema Sepetu ‘Madam.
Alipotafutwa Aunt na kuulizwa kama kweli ndiyo wamefikia hatu hiyo na
Wema, alikiri kufikia hatua ya kutamka kauli hiyo kwani anashindwa
kumuelewa shosti wake huyo ana kitu gani moyoni ambacho kimemfanya
ashindwe kumtembelea tangu ajifungue.“Nashindwa kumuelewa Wema sijui kuna kitu gani kikubwa kinachomfanya ashindwe kumuona mwanangu na sisi tulikuwa marafiki. Siwezi kwenda katika sherehe yake katika hali kama hii tuliyonayo labda kwa ishu ya msiba, nitaennda,” alisema Aunt.Kwa upande wake Wema alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, hakuwa tayari kuzungumzia lolote.

Note: Only a member of this blog may post a comment.