Kila mmoja anamfahamu vizuri Cristiano Ronaldo ambaye anakipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Ureno. Ronaldo ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2003 na kutimkia Real Madrid mwaka 2009 anaikumbuka kwa furaha siku kama ya leo akiwa na Man United.
Cristiano Ronaldo anaikumbuka siku ya November 1 mwaka 2003 ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kufunga goli akiwa na Man United, Ronaldo
alifunga goli hilo kwa mpira wa faulo ambao ulitinga wavuni moja kwa
moja na kuandika historia hiyo ambayo leo November 1 ni siku ya
kumbukumbu yake.
Goli hilo la Cristiano Ronaldo alifunga katika mechi dhidi ya Portsmouth
goli ambalo lilianza kumpa heshima kutokana na namba ya jezi namba saba
aliyokuwa anavaa ilikuwa imeachwa na mchezaji mahiri kipindi hicho David Beckham ambapo alitimkia Real Madrid staa huyo.
Hii ni video ya goli la kwanza la Cristiano Ronaldo akiwa na Man United goli ambalo alilifunga November 1 2003.
Note: Only a member of this blog may post a comment.