Jezi namba 7 ni miongoni mwa jezi zenye heshima kubwa katika klabu ya
Manchester United na moja kati ya watu walioipatia heshima jezi hiyo ni
David Beckham na Cristiano Ronaldo.
Memphis Depay aliyesajiliwa msimu huu na klabu ya Manchester United
akitokea PSV Endhoven ya Uholanzi kwa dau la pound milioni 25 ambaye ndo
anavaa jezi hiyo kwa sasa.
Depay ambaye kwa wiki za karibuni amekuwa akikaa benchi na mchezaji
Jesse Lingard kuchukua nafasi yake, inatajwa kuwa na presha kubwa
kutokana na wengi kutaka kuona anaifanyia makubwa jezi namba 7 kama
walivyofanya Cristiano Ronaldo na David Beckham.
David Beckham amempa ushauri Memphis Depay kuwa hatakiwi kuwa na
presha au kuogopa kuvaa jezi hiyo licha ya kuwa inatajwa kuwa na
mafanikio makubwa Man United lakini ni heshima kwake kuvaa jezi namba
saba.
“Sioni kama jezi namba 7 inatisha au kuogopesha chochote mimi
nafikiria ni heshima kuivaa, unapopewa jezi namba 7 haina maana ya
kwamba hadi uwe umeshinda au huyo mchezaji awe amepata mafanikio sana,
lakini mwisho wa siku ni jezi maalum kuivaa ila sifikirii kama inakuwa
na presha kuivaa binafsi ni jezi inayonihamasisha uwanjani” >>>
Beckham
Note: Only a member of this blog may post a comment.