Majimbo mawili ya Rushoto mkoani Tanga pamoja na lile la Ulanga
mashariki mkoani Morogoro kesho November 22 yatakuwa katika uchaguzi wa
kuwachagua wabunge watakao wawakilisha kwenye bunge la 11 la jamuhuri
ya muungano wa Tanzania , hii ni baada ya wagombea wa majimbo hayo
kufariki kabla ya uchaguzi mkuu uliofanyika October 25.
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC uchaguzi wa nafasi ya
mbunge katika jimbo husika utalazimika kurudiwa endapo mmoja kati ya
wagombea atafariki kabla ya uchaguzi kufanyika.
Hapa kaimu mkurugezi wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe ametoa ratiba nzima na taratibu za kufuata kwa wapiga kura wote>>>
“Vituo vitafunguliwa saa 1 kamili
asubuhi na kufungwa saa 10 kamili za jioni, iwapo wakati wa kufunga
kituo kukawa na watu waliokatika foleni na walifika kabla ya saa 10
watapata nafasi ya kupiga kura”
Baada ya kupiga kura taratibu gani itafuata? Kalieleza na hili>>
“Matokeo yote yakishapokelewa na
msimamizi wa uchaguzi yatajumlishwa mbele ya mawakala na watu wote
wanaoruhusiwa, baada ya kuhesabu kura fomu zitatiwa saini na mawakala
watakaokuwepo.”
Hapa nimekuwekea sauti yake unaweza kuisikiliza>>>
Note: Only a member of this blog may post a comment.