Friday, November 20, 2015

Anonymous

Rais OBAMA na Uvutaji wa Sigara Ikulu...Je, Akiwa na Mkewe Wanakula Raha Huwa Anaweza Kupokea Simu ya Nani?! Majibu Yote Aliyojibu Yapo Hapa....

Rais Barack Obama anakaribia kumaliza muhula wake wa pili kuiongoza Marekani tangu mwaka 2008, lakini kuna tabia yake aliyokuwa nayo muda mrefu ya kuvuta sigara… alipoingia White House aliendelea kuvuta?
Obama alihojiwa na kwenye sentensi za kwanza kajibu hivi >>> “Sijavuta sigara hata moja ndani ya miaka mitano tangu nimeingia Ikulu… Niliahidi kwamba Muswada wa Sheria mpya ya Afya ukipita (2010) sivuti tena sigara, na kweli imetimia“.

Obama anasema alijaribu mara kadhaa kuachana na sigara mwaka 2008 wakati wa Kampeni  za Urais lakini ilishindikana, kuna wakati alijikuta akijibana zake kona na kuvuta tena na tena !!
Unajua kingine alichojibu Rais Obama kuhusu kuacha kuvuta sigara >>> ‘Namuogopa mke wangu’… Michelle kumbe nae hakuipenda tabia ya uvutaji sigara ya Obama iendelee !!
Achana na hayo, swali jingine la kizushi kwa Obama… akiwa zake ‘out’ na Michelle wake wanakula raha, simu ya nani anaweza kupokea ikiita? >>> “Mmmmh… labda ya Malia, Sasha (watoto wake) na mama mkwe.. nyingine ya mshauri wangu wa usalama Susan Rice, na Katibu Mkuu Kiongozi,  Denis McDonough” >>> Barack Obama.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.