Komediani maarufu Bongo, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’.
Imelda mtemaPole! Komediani maarufu Bongo, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ amesema kuwa matokeo ya uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kisarawe ambapo alikuwa mmoja wa wagombea, yamemfanya kupata ugonjwa wa presha baada ya kuwa ameshindwa.
“Uchaguzi usikieni tu, siyo kitu cha mchezo hata kidogo. Mimi hapa nimepata ugonjwa wa presha. Pamoja na kukosa lakini najipanga upya kipindi kijacho nitagombea tena baada ya kusomea siasa,” alisema Kingwendu aliyekuwa akigombea kwa tiketi ya Chama cha CUF akiungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Note: Only a member of this blog may post a comment.