
Katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC imefanikiwa kileleni mwa msimamo baada ya kuibugiza Toto Africans ya Mwanza magoli 5-0 yaliyofungwa na Shomari Kapombe (2) Didier Kavumbagu (2) na Kipre Tchetche.
Huko Tanga wanakimanumanu African Sports wamekubali kichapo cha magoli 2-0 toka kwa JKT Ruvu wakati huko Mbeya, wenyeji Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya 2-2 na Ndanda FC ya Mtwara. Kwa habari hizo na nyinginezo usikose kuangalia kipindi cha Mshikemshike cha Azam Tv kuanzia saa 2.30 usiku huu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.