Katika mkutano huo Mwenyekiti wa chama hicho Anna Mgwhira alitumia nafasi hiyo kuweza kuwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kuwasuport katika kipindi chote cha kampeni na kukifanya chama kuzidi kuwa imara zaidi.
Zitto Kabwe naye alizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo kumpongeza Mwenyekiri wake Anna Mgwhira kwa kumsaidia kukitangaza chama hicho na kupandisha taswira ya chama chao mbele ya umma.
“Kazi iliyopo mbele yetu ni kukijenga chama na kukifanya kifike mbali zaidi, tumefanikiwa kupata kiti kimoja cha ubunge lakini tutatumia kiti hicho kupaza sauti ndani ya bunge..ikumbukwe sisi tulisema waziwazi kuhusu rushwa tofauti na vyama vingine vya upinzani ambavyo havikuwa wazi”..Zitto
Pia alizungumzia suala ya dawa za kulevya“Nchi nyingi zimeanza kufanya mabadiliko kuhusu dawa za kulevya, dunia nzima imeanza mkakati wa kupambana na dawa za kulevya, ujangili pamoja na rushwa ambayo ndio mambo tutakayokwenda nayo ndani ya bunge ili kuweza kupaza sauti zetu ndani ya jamii inayotuzunguka”..
Pia alimpongeza Rais Dk.Magufuli kwa kuweza kudhibiti safari za nje“Wakati nikiwa Mwenyekiti wa PAC niliagiza kufanywa ukaguzi wa fedha za umma kuhusu safari za nje za viongozi wetu, nataka tu niwahahakikishie Watanzania wenzangu mimi na marehemu Deo FILIKUNJOMBE tuliagiza ukaguzi na upo tayari, wakati wowote tutawaita na kulitolea maelezo ya kina”.
“Kwenda tu katika sehemu na kushtukiza hakutatatua wizi wa mali za umma, tunataka Rais aweke mifumo endelevu ili leo na kesho akiwa hayupo iweze kufanya kazi kwa manufaa ya umma”.
Kuhusu mgogoro wa Zanzibar Zitto amesema “ZEC imefuta uchaguzi lakini ukisoma katiba ya Zanzibar hakuna mahali panaonyesha Mwenyekiti wa Zanzibar ana mamlaka ya kufuta uchaguzi, kama tatizo lilikuwa ni majimbo ya Pemba tume ilipaswa kurudia kuhesabu kura kwenye yale majimbo husika”.
“Mpaka leo tunapozungumza kikatiba Zanzibar haina Serikali, mtu yeyote anayejiita rais wa Zanzibar kikatiba amepindua, anapaswa kushtakiwa kwa kosa la kiuhaini na kosa lake adhabu yake ni kifo, tunamtaka Rais Magufuli ahakikishe tume ya ZEC inatangaza matokeo”.
Note: Only a member of this blog may post a comment.