Mwalimu Mkuu huyo alivyonaswa siku ya tukio.
Issa Mnally
Jambo limezua
jambo! Habari ikufikie kwamba Wizara ya Elimu nchini inamshughulikia
yule Ticha Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa iliyopo Upanga
jijini Dar (jina tunalo) ambaye hivi karibuni alinaswa na makamanda wa
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers akiwa ofisini kwake
na mke wa mtu ambaye ni mzazi wa mwanafunzi wake.
Katika habari hiyo part one, hii ikiwa
ni part two, iliyoripotiwa na gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko,
mwalimu huyo alinaswa ofisini kwake na mzazi huyo huku walichokuwa
wakitaka kufanya ikiwa ni siri yao.
Kwa mujibu wa habari hiyo, mzazi wa
mwanafunzi huyo alimwambia mwandishi wetu kuwa mwalimu huyo alimpigia
simu na kumwita aende shuleni hapo wakaongee lakini hakwenda kwa kuhofia
usalama wake.
Siku ya tukio hilo, OFM, wakiwa katika
harakati za kutafuta habari walifika shuleni hapo na kukuta kuna kikundi
kidogo cha watu na walipojipenyeza ndani walimkuta mwalimu mkuu huyo
akiwa katika harakari za kufunga zipu.
Pamoja na fedheha hiyo, mapema wiki hii
wanahabari wetu walifika shuleni hapo na kumkuta mkuu huyo wa shule
akiendelea kuchapa mzigo kama kawaida ndipo wakatinga wizarani kujua
kama kuna hatua zozote zilikuwa zimechukuliwa dhidi yake.
Hata hivyo, waandishi wetu walipofika
wizarani walielezwa kwamba tayari maelekezo ya namna ya kumshughulikia
mwalimu huyo yalikuwa yametolewa kwa Afisa Elimu wa Mkoa wa Kielimu wa
Ilala aliyetajwa kwa jina moja la Mapunda.
Gazeti hili lilipofika kwa afisa huyo wa
elimu alisema kuwa kosa hilo ni kubwa hivyo ni lazima mwalimu huyo
achukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kutimuliwa kazi kwa mujibu wa
maelekezo ya Wizara ya Elimu.
“Tumeagizwa kufanya uchunguzi,
ikibainika kweli ametenda kosa hilo lazima hatua za kinidhamu
zichukuliwe dhidi yake,” alisema Mapunda.
Katika tukio hilo, mwalimu huyo alipigwa
pingu na polisi ambapo alipelekwa kwenye kituo cha polisi kilicho
karibu na eneo hilo hilo kabla ya kuachiwa baada ya kuchukuliwa maelezo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.