Lori lenye kontena ambalo halijafungwa vizuri likiwa barabarani.
Dereva akiendelea na safari bila kujali hatari yoyote.
Safari ikiendelea.
Katika hali isiyo ya kawaida, Lori lenye
namba za usajili T 498 AHS lililokuwa limebeba kontena katika barabara
ya Kilwa, kuelekea barabara ya Bandari/Shimo la Udongo ambalo lilikuwa
halijafungwa vizuri na kuonekana kuyumba bila wahusika kuchukua hatua
yoyote hivyo linaweza kusababisha hatari kwa watumiaji wengine wa
barabara ikiwemo kupelekea ajali.
Mara kadhaa zimekuwa zikiripotiwa ajali
zinazotokana na malori yaliyobeba makontena kuanguka na mengine
kudondokea watu na kusababisha uhalibifu wa mali na wakati mwingine
vifo.
Je, kwa hali hii kweli ajali za namna hii zitaisha nchini?
(Picha na Global Whatsapp 0753 715 779, kama una tukio lolote usisite kututumia kupitia namba hiyo)
Note: Only a member of this blog may post a comment.