KUMEKUCHA! CCM YAANZA MCHAKATO WA KUMTAFUTA MGOMBEA JIMBO LA HANDENI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Wanahabari wakichukua tukio.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Nape akijiandaa kujibu maswali ya wanahabari yaliyokuwa yameulizwa (hawapo pichani).
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kipo kwenye mchakato wa kumtafuta
mgombea wake wa Ubunge Jimbo la Handeni mkoani Tanga baada ya
kutofanyika uchaguzi kufuatia kifo cha mgombea wake kwa tiketi ya chama
hicho, Abadallah Kigoda.
Akizungumza na wanahabari leo kwenye ofisi za chama hicho zilizopo
mtaa wa Lumumba jiijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye amesema kuwa, wajumbe wa kamati ya CCM wapo kwenye mchakato huo
na kesho mgombea atapatikana.
Alisema kamati hiyo imeshachuja waliojitokeza kuomba nafasi hiyo
ambao walikuwa 11 na sasa wamebaki wawili ambao ni Hamis Hamad na Omar
Kigoda hivyo kesho watakaa kikao cha kumpata mgombea mmoja.
NA DENIS MTIMA/GPL
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.