Na Waandishi Wetu
ZIARA mbili tu
alizofanya Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ kwenye Wizara ya Fedha na
kukuta wafanyakazi sita wamekwenda ‘brekfasti’ na ile ya Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) na kukuta mashine za MRI na CT Scan ziko hoi,
tayari nchi imetikisika ambapo sasa kila mtumishi wa serikali analinda
kibarua chake kwa kufuata masharti ya ajira.
Kufuatia ‘shtukiza’ hizo, sasa kila mkuu
wa kitengo kwenye ofisi za serikali, anasimamia vyema uadilifu na
wafanyakazi wake kwa kuwa ‘hawajui siku wala saa’ ambayo Magufuli
ataibukia hapo.
Novemba 10 na 11, mwaka huu, timu ya
waandishi wa gazeti hili ilidamkia kwenye wizara mbalimbali zilizopo
jijini Dar kwa lengo la kujionea wafanyakazi wanavyowahi au kuchelewa
katika kipindi hiki cha ‘Hapa Kazi Tu’.
Pia, Uwazi ilitaka kujua kama makatibu
wakuu wa wizara hizo ambao kwa sasa ndiyo wasimamizi wakuu baada ya
kutokuwepo kwa mawaziri, wanawahi maofisini au bado wanakwenda kwa
‘mwendo wa kizamani’.
Saa moja na nusu juu ya alama, Uwazi
lilitia timu kwenye Wizara ya Ujenzi kwenye makao yake makuu maeneo ya
Posta na kukuta katibu mkuu wake, Mhandisi Mussa Iyombe ameshafika ‘siku
nyingi’. Gari la katibu huyo lilikuwa kwenye maegesho.
Mwandishi wetu aliweza kupiga picha,
lakini kabla hajatoka, alitiwa mbaroni na walinzi wa wizara hiyo baada
ya simu kupigwa getini na kujulishwa kuwa, kamera za ulinzi (CCTV)
zimemwona mtu akipiga picha.
Hata hivyo, baadaye walinzi hao walimwachia mwandishi huyo kwa vile hakuwa na silaha yoyote.
Mwandishi mwingine, muda huohuo alivamia
Wizara ya Habari, Utamaduni Vijana na Michezo iliyopo Posta ambapo
katibu mkuu wake ni Profesa Elisante Ole Gabriel na kuambiwa na walinzi
kuwa, bosi huyo alikwishakaa kwenye kiti chake.
Jengo la Wizara ya Maliasiri na Utalii
Jengo la Wizara ya Uchukuzi
Ili kuendelea kujiridhisha na uchunguzi
wake, Uwazi liliibukia Wizara ya Uchukuzi maeneo ya Posta na kumkuta
Katibu Mkuu, Shaaban Mwinjaka ameshapita langoni kuingia ofisini kwake.
Siku ya pili, Uwazi likajihimu kwenda
Wizara ya Maliasili na Utalii maeneo ya Keko na kuambiwa na mlinzi kuwa,
Katibu Mkuu, Dk. Adelhelm Meru hajafika. Uwazi lilipiga kambi lakini
katika hali ya kushtukiza, ndani ya dakika kumi aliingia na kuwahi muda
wa kuingia kazini kwa watumishi wa serikali ambao ni saa 1:30 mpaka saa
2:00 asubuhi
Uwazi lilibahatika kuzungumza na katibu mkuu huyo ofisini kwake kwa kumuuliza kuhusu maendeleo ya Hoteli ya Embassy iliyopo maeneo ya Posta ambayo mmliki wake ni wizara hiyo. Katibu mkuu huyo alikuja mbogo akimwambia mwandishi hawezi kujibu swali hilo kwani yeye anajua kila kitu.
Pia, Mwandishi mwingine wa Uwazi aliwasili kwenye Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii lakini katibu mkuu wake, Donald Mmbando alishafika na mlinzi aliweka ngumu kumwona kwa madai kwamba tayari alikuwa kwenye kikao cha kila siku na wafanyakazi wa wizara hiyo.
Uwazi lilibahatika kuzungumza na katibu mkuu huyo ofisini kwake kwa kumuuliza kuhusu maendeleo ya Hoteli ya Embassy iliyopo maeneo ya Posta ambayo mmliki wake ni wizara hiyo. Katibu mkuu huyo alikuja mbogo akimwambia mwandishi hawezi kujibu swali hilo kwani yeye anajua kila kitu.
Pia, Mwandishi mwingine wa Uwazi aliwasili kwenye Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii lakini katibu mkuu wake, Donald Mmbando alishafika na mlinzi aliweka ngumu kumwona kwa madai kwamba tayari alikuwa kwenye kikao cha kila siku na wafanyakazi wa wizara hiyo.
“Unajua siku hizi huwezi kukuta katibu
mkuu amechelewa. Magufuli anawahenyesha ile mbaya. Sasa kama mtu hataki
kazi, achelewe aone,” alisema mfanyakazi mmoja wa wizara hiyo bila
kutaja jina lake.
Note: Only a member of this blog may post a comment.