Watoto wa familia ya mzee Michael Mgunda (72) wakiwa nje ya Kituo cha Afya cha Mselem (Mselem Medical Center), Kipunguni, Dar
Stori: Chande Abdallah na Suzan Kayogela
WATOTO wa familia ya mzee Michael Mgunda (72) wametinga katika Kituo cha Afya cha Mselem (Mselem Medical Center), Kipunguni, Dar wakidai kudhulumiwa gharama za matibabu za mgonjwa wao mzee huyo mwenye tatizo la kibofu cha mkojo.
WATOTO wa familia ya mzee Michael Mgunda (72) wametinga katika Kituo cha Afya cha Mselem (Mselem Medical Center), Kipunguni, Dar wakidai kudhulumiwa gharama za matibabu za mgonjwa wao mzee huyo mwenye tatizo la kibofu cha mkojo.
Tukio hilo lilijiri Novemba 11, mwaka
huu ambapo ndugu hao walidai awali walimpeleka mgonjwa wao katika kituo
hicho ili afanyiwe operesheni lakini walishangaa wakitozwa gharama
nyingi ikiwa pamoja na nyingine zisizo na maana lakini mgonjwa wao
hakutibiwa.
Gharama walizolipia katika Kituo cha Afya cha Mselem (Mselem Medical Center)
Akizungumza na Amani, mtoto wa mzee
huyo, Rashid alisema moja kati ya gharama walizodai kutozwa kiholela ni
mgonjwa wao kuwekewa dripu nne, kuchomwa sindano mbili ambazo zinadaiwa
hazikuhusika na tatizo la mgonjwa huku akiachwa bila kufanyiwa upasuaji.
“Gharama zote zilifika shilingi laki
moja na elfu sitini na saba (167,000). Nilishangaa siku ya pili nakwenda
kumchukua mgonjwa namkuta akiwa katika hali mbaya halafu hajafanyiwa
upasuaji. Nikamfuata daktari kumuuliza lakini hakunipa majibu sahihi,
ndiyo nikataka nirudishiwe gharama zangu,” alisema Rashid.
Hata hivyo, alidai wakati anafuatilia
fedha zake alizungushwa kwa muda wa siku tano akiambiwa angerudishiwa
shilingi 50,000 tu tena kwa njia ya mtandao ambapo alidai hajapata fedha
hizo mpaka hivi karibuni (alipozungumza na gazeti hili) huku
wakilazimika kumpeleka mgonjwa wao Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako
alitibiwa kwa shilingi elfu 50,000.
Amani liliwatafuta wahusika wa hospitali
hiyo ambao walikiri kumpokea mgonjwa huyo tarehe husika na kutomfanyia
operesheni lakini walisema wameshamlipa Rashid kiasi hicho cha pesa
alichokuwa akidai lakini wanashangaa akiendelea kuwadai.
“Huyu mgonjwa tunamjua lakini hayo madai
ya mtoto wake kuwa hatujamlipa si ya kweli. Tulishamlipa kwa mtandao na
meseji tulimuonesha. Sasa kwa nini hakubali hilo, tunashangaa anakuja
na RB ambayo pia tuna shaka nayo,” alisema mtunza fedha wa kituo hicho,
Mwanahawa Ali.
Note: Only a member of this blog may post a comment.