Akitangaza
nafasi hizo jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhani Kailima alisema kuwa
uteuzi huo wa nafasi hizo huzingatia moja ya tatu ya idadi ya kata
zilizopo kwenye halmashauri au manspaa ya jiji husika.
Kailima
alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 35(I)(C)sura ya 287,kifungu cha
19(I)(C) sura ya 288 zikisomwa pamoja na kifungu cha 86A sura 292 za
sheria za serikali za mitaa, Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ikitwaa
jumla ya viti 365,kwa Chadema kutwaa viti 280,CUF viti 79 na NCCR
mageuzi kutwaa viti sita ,ambapo Chama cha Mapinduzi CCM ikipata viti
1022, na chama cha ACT-Wazalendo ikitwa viti sita.
“Tuna
vitaka vyama vya siasa vituletee majina ya madiwani wao ili
kuharakaisha shughuli za mabaraza ya halmashauri ambapo kisheria ni kila
baraza likinatakiwa lianze kufanya shughuli zake siku 30 baada ya
uchaguzi,”alisema Kailima.
Wakati
huo huo Mkuregenzi huyo wa uchaguzi alitaja siku za kufanyika kwa
uchaguzi wa majimbo ambao uchaguzi wake uliohairishwa kutokana na
kufariki kwa wagombea na sababu nyengine zakisheria.
Alieleza
kuwa jimbo la Lushoto na Ulanga Mashariki utafanyika Novemba 22,jimbo
la Arusha Mjini na Handeni utafanyika Desemba 13 ambapo jimbo Ludewa na
Masasi Mjini utafanyika Desemba 20
Note: Only a member of this blog may post a comment.