Ni headlines za staa wa soka anayeipeperusha vyema bendera ya Sweden na anakipiga katika klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic, ameingia katika headlines kadhaa mwaka 2015 ikiwemo kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Sweden kwa mara ya tisa mfululizo na mara 10 kwa jumla.
November 27 mkali huyo wa Sweden
ametangaza kuanzisha mtandao maalum ambao utakuwa unawekwa video na
taarifa za magoli yake katika historia yake ya soka toka yupo Malmo, Ajax na vilabu vingine pamoja na magoli yake aliyoshinda akiwa na timu yake ya taifa ya Sweden. Mtandao wa Zlatan unaitwa “Zhowtime” jina ambalo limetungwa na waandishi wa habari wa Sweden.
Watafiti wa Zlatan
wametumia mwaka mzima kuandaa na kutafuta magoli ya staa huyo ambayo
utakuwa unaweza kutafuta kwa msimu na Ligi, katika mtandao huo utapata
kuona magoli zaidi ya 300 aliyofunga kwa ngazi ya klabu na zaidi ya 50
kwa timu yake ya taifa ya Sweden, huu ni utaratibu
mwingine wa staa huyo wa kutunza kumbukumbu zake baada ya kuzoea kumuona
akitumia mwili wake kama sehemu ya kutunza kumbukumbu zake muhimu kwa
michoro ya tattoo.
Video ya moja kati ya magoli makali ya Zlatan Ibrahimovic
Note: Only a member of this blog may post a comment.