Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake, Rais Jakaya Kikwete ni
kiongozi ambaye kwenye vitu atakavyokumbukwa kwa kuvifanya wakati wote
wa uongozi wake ni juhudi zake kwenye kuinua Michezo TZ.
Ili Tanzania ifanye vizuri kwenye
michezo kazi kubwa bado inatakiwa kufanyika, kinyume cha hapo hakuna
miujiza itakayokuja kubadili hali na kuipandisha zaidi michezo.
October 17 2015 Rais JK alizindua Kituo maalum cha kukuza vipaji vya watoto kilichojengwa katikati ya Jiji Dar es Salaam eneo la Kidongo Chekundu… hiyo ni hatua nyingine nzuri kwamba uwekezaji wa vipaji unatakiwa kuanzia kwenye ngazi ya watoto.
Kama hujabahatika kupaona, unaweza kucheki hizi pichaz Kituo cha Michezo Kidongo Chekundu kwenye ubora wake yani.

Kwenye Kituo hicho watoto wanajifunza michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu, Basketball na Volleyball.
Muonekano mwingine wa viwanja ndani ya Kituo hicho huu hapa
Note: Only a member of this blog may post a comment.