Friday, November 20, 2015

Anonymous

2 VIDEOS: Wabunge Wa UKAWA Walivyozomea na Kutolewa Nje ya Bunge Leo

Wabunge  wanaounga  umoja  wa  Katiba  Ya  Wananchi, UKAWA  wametolewa  nje  ya  ukumbi  wa bunge leo baada  ya  kugoma  kutambua  ujio  wa  Dr Shein bungeni  na  kuanza  kuzomea  huku  wakisema  Maalim Seif....Maalim Seif
 
Wabunge hao awali walitoa msimamo wao wa kutokubali Dk Ali Shein kuhudhuria Bunge hilo wakati rais atakapoingia Bungeni kulihutubia Bunge kwa kuwa hawamtambui kama rais wa Zanzibar kwani kwa mujibu wa Katiba muda wake umekwisha.

Kelele za zomeazomea ziliibuka ghafla wakati Rais  Dk Shein alipoingia bungeni hali iliyoondoa utulivu wa Bunge.

Hata hivyo, Mbunge pekee wa upinzani, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo) alibaki ndani ya Bunge kwa utulivu na kuendelea kusikiliza hotuba ya Rais.

Awali, wabunge hao walimuandikia barua Spika wa Bunge wakihoji uhalali wa hotuba ya Rais bungeni endapo Dk Shein atahudhuria Bunge hilo kama Rais wa Zanzibar.

Ukawa wameendelea kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (NEC) kumtangaza mshindi wa nafasi ya Urais wa Zanzibar, huku mgombea wa CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akidai kuwa ameshinda kutokana na kura halali alizokusanya kwenye vituo vyote. 

Spika  wa  bunge,Job Ndugai  aliwataka  wabunge  hao waache kuzomea  na  badala  yake  wakae chini  lakini  wakakaida, hali  iliyomfanya  awaamuru  watoke  nje kwa  hiari  yao  kabla  nguvu  ya  dola  haijatumika  kuwatoa.
Tazama na hizi video mbili hapa

Baada ya kuombwa mara tatu na Spika wa Bunge, wabunge kutoka vyama vya upinzani waamuriwa kutoka nje ya Bunge kutokana na kuanzisha mzozo Na tafaruku punde tu alipotambulishwa Dr Shein kama Rais wa Zanzibar.Kutoka Bungeni Live #azamTWO fuatilia Rais Magufuli akihutubia Bunge la 11.

Posted by Azam TV on Friday, November 20, 2015

DR. ALI MOHAMED SHEIN APOKEWA NA ZOMEA ZOMEA KUTOKA KWA WABUNGE WA UPINZANI WAKATI WA UZINDUZI WA BUNGE LA KUMI NA MOJAMustakabali wa wa demokrasia Tanzania bado ni kitendawili kufuatia Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutoa tamko la kufuta uchaguzi wa Zanzibar.#HABARI Aliyeingia hivi sasa Bungeni katika uzinduizi wa Bunge ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein,kelele nyingi zinasikika kutoka kwa wabunge wa UKAWA wakipinga kutomtambua huku wakilitaja jina la Maalim SeifKelele za wabunge zinaimba "Maalif Seif, Maalim Seif, Maalim Seif, Maalim Seifu..." Lakini taratibu zinaendeleaSpika wa Bunge Job Ndugai amewaamuru wabunge wanaopiga kelele watoke nje. Askari wameingia na kuwaamuru wabunge watoke nje, wabunge wote waliokuwa wakipiga kelele wametoka njeQuote : Magufuli...nitashirikiana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na hasa viongozi wa vyama vya CCM na CUF kuhakikisha hali iliyopo sasa Zanzibar inapatiwa muafaka kwa haraka..... - Dk. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania #BungeniDodoma.

Posted by Zanzibar Post on Friday, November 20, 2015

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.