
Wema Isaac Sepetu akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Tunakukumbuka Mwalimu! Beautiful Onyinye kwenye sinema za Kibongo, Wema
Isaac Sepetu kupitia Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao, amejikuta akimwaga
chozi kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.
Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita baada ya mrembo huyo na mastaa
wenzake walipotembelea kaburi hilo lililoko kijijini kwake, Butiama
Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Wasanii wakiwa katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao imelenga kuzunguka mikoa mbalimbali nchini kuwahamasisha akina mama ili wawashawishi vijana wao kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Baadhi ya mastaa wa Bongo Movies walioongozana na Wema ni pamoja na Salome Urassa ‘Thea’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’, Mayassa Mrisho ‘Maya’ Sabrina Rupia ‘Cathy’ na wengine kibao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.