Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yuko jijini Arusha ambapo jioni hii yupo katikati ya jijini hilo ndani ya uwanja wa Sheikh Amir Abeid, akinadi sera za chama chake. 
Kabla ya kufanya mkutano kwenye uwanja wa Sheikh Amir Abeid jioni hii, Dk. Magufuli alielekea kwanza wilayani Monduli leo asubuhi ambako alitakiwa kufanya mkutano wa hadhara katika eneo la Mto wa Mbu kwa mujibu wa ratiba yake.
Taarifa tulizozipata zinaarifu kuwa hali haikuwa nzuri katika eneo hilo la Mto wa Mbu baada ya msafara wake kukumbana na wafuasi wa UKAWA ambao walivamia msafara huo na kuanza kushangilia wakisema Lowassa!!!....Lowassa!! Lowassa!!! huku wakiwa wamenyoosha vidole viwili juu.-Tazama Video Hii

Hali hiyo iliwafanya polisi waingile kati kwa kupiga mabomu ya machozi ambapo vijana kadhaa wametiwa mbaroni wakituhumiwa kuhujumu mkutano huo wa Magufuli.- Tazama na Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.