Friday, October 2, 2015

Anonymous

VITA YA NDUGU! ESMA Ampa za Uso DIAMOND PLATINUMZ

ESMA.jpg 
Brighton Masalu
DADA wa ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma amemshangaa kaka yake, (Diamond) kwa kuendeleza chuki dhidi ya baba yake mzazi, mzee Abdul Jumaa.
diamond1
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu hivi karibuni, Esma alisema siku zote si vyema kukaa na kinyongo au chuki dhidi ya wazazi na hata kama ikitokea ni vyema kuyamaliza kwa mtoto kujishusha.
“Hata mimi nilishawahi kukosana na baba yangu, lakini nilishasamehe na kusahau kabisa, hata hapa nyumbani, ni mara nyingi tu huwa tunatofautiana na mama lakini hata kama yeye kakosea, huwa najishusha si kama ilivyo kwa Nasibu (Diamond) kuwa na chuki kali kiasi hicho dhidi ya baba yake,” alisema Esma.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.