Imelda Mtema
HEE! Staa
kiwango kunako tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel hivi karibuni
alishindwa kupata usingizi kufuatia kuangua kilio sababu ikiwa ni
kumkumbuka mtoto wake, Cookie ambaye hajamuona kwa zaidi ya mwezi mmoja
sasa kutokana na kubanwa na misafara ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Akizungumza kwa uchungu, Aunt alisema,
japokuwa yupo kwenye kampeni hizo lakini kila wakati anamkumbuka mtoto
wake kwa kuwa alimuacha muda mrefu na yeye akiwa kama mama mwenye
uchungu lazima ifike wakati amkumbuke mtoto wake huyo.
“Mara nyingi sipati usingizi kwa
kumuwaza Cookie. Kama leo sijalala kabisa, nilikuwa nalia kwa ajili
yake. Nimemkumbuka sana mwanangu. Hii yote ni kwa ajili ya kazi na
kumtafutia maisha bora ndiyo maana nikaamua kumuacha na baba yake,”
alisema Aunt.

Note: Only a member of this blog may post a comment.