Tuesday, October 20, 2015

Anonymous

TAARIFA: Rais JK Afanya Uteuzi Mpya Kwenye Mahakama!

RAIS KIKWETE
Rais Jakaya Kikwete.
IKULU MAWASILIANO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi katika Mahakama kama ifuatavyo;
Rais amemteua Bi. Katarina Revocati kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (Chief Registrar). Kabla ya uteuzi huu, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. 
Rais pia amemteua Ndugu John Rugalema Kahyoza kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani na kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kahyoza alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu.
Mwingine aliyeteuliwa ni Ndugu Ilvin Claud Mugeta ambaye anakuwa Msajili wa Mahakama Kuu. Kabla
ya Uteuzi huu ndugu Mugeta alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi na Maadili.
 

Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Oktoba, 2015.
Imetolewa na:  
Premi Kibanga,  
Mwandishi wa Habari wa Rais, 
Msaidizi Ikulu,  
DAR ES SALAAM.  
19 Oktoba, 2015.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.