STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena
Mohamed ‘Shilole’ ametoboa siri ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi
wake Naftari Mlawa ‘Nuh’ akisema alifanya hivyo ili kumpa imani
mwanaume huyo kuwa anampenda sana.
Akizungumza na gazeti hili juzikati,
Shilole alisema siku zote mpenzi wake hakuwa akiamini kama anampenda,
licha ya ukweli kwamba naye alikuwa amechora tattoo yenye jina lake.
“Nuh alikuwa haamini kama kweli nina
mapenzi ya dhati kwake, niliamua kuchora tattoo ya jina lake na sasa
ameamini nampenda, mapenzi yetu yameimarika kuliko mwanzoni, amejiona ni
mtu muhimu sana kwangu, kwani hata mwanaume yeyote akiona nimejichora
jina hili, lazima ashtuke na aone kwamba nina mtu tunayependana,”
alisema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.