Thursday, October 15, 2015

Anonymous

PICHAZ: Shuhudia Balozi MWAPACHU Akirudisha Rasmi Kadi ya CCM

Mwapachu 2 mwapachu 3
Balozi Mwapachu (kulia) akikabidhi kadi yake ya uanachama wa CCM kwa Katibu wa Siasa na Uenezi CCM, mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba.
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu leo amerejesha kadi yake ya uanachama ofisi za chama hicho zilizopo Mikocheni A jijini Dar es Salaam.
Balozi Mwapachu aliyetangaza kukihama chama hicho juzi (Jumanne) kwa madai kuwa kimepoteza dira, amekabidhi kadi hiyo kwa Katibu wa Siasa na Uenezi CCM, mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba.
Mwanasiasa huyo ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa miaka 48 alisema bado hajaamua ahamie chama gani.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.