Thursday, October 22, 2015

Anonymous

PICHAZ na MATOKEO ya Mechi Zote za Ligi Kuu Tanzania Bara VPL Jana Nimekuwekea Hapa!


Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea tena leo Otcober 21 kwa timu 10 kushuka uwanjani kuwania point tatu muhimu, point ambazo zitaisadia kila timu kuwa katika nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2015/2016, msimu ambao kila timu inaonekana kuleta ushindani mkubwa katika kila mechi.

Kikosi cha Yanga
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara Dar Es Salaam Young African, walishuka dimbani katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kuwakaribisha Toto African ya Mwanza, huu ukiwa ni mchezo wa saba kwa Yanga wakati kwa upande wa Toto African ambao walikuwa nafasi ya nane katika msimamao wa Ligi Kuu Tanzania bara ni mchezo wao wa nane.

Kikosi cha Toto African
Dar Es Salaam Young African ambao bado hawajapoteza mchezo hata mmoja kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu, wameendeleza wimbi la ushindi kwa kuifunga Totot African kwa jumla ya goli 4-1. Magoli ya Yanga yalifungwa na Juma Abdul dakika ya 9, Simon Msuva dakika ya 48 na 90, Amissi Tambwe dakika ya 81 huku goli pekee la Toto African lilifungwa na Miraji Athumani dakika ya 55.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania bara zilizochezwa October 21
Stand United 3 – 0 Maji Maji FC
Coastal Union 1 – 0 Kagera Sugar

Tambwe akiwania mpira na Hamisi Kasanga

Juma Abdul akijaribu kumtoka Robert Magadula

Haruna Niyonzima akipiga krosi

Simon Msuva akijaribu kumtoka beki wa Toto

Donald Ngoma akijaribu kupiga krosi iliyozuiliwa na Hamis Kasanga

Niyonzima na Juma Abdul wakishangilia goli lao la kwanza

Simon Msuva akishangilia na Coutinho baada ya kufunga goli

Amissi Tambwe akishangilia goli na Simon Msuva

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.