Richard Bukos
Mambo ya uchaguzi! Ama kweli nyota ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Baba Tiffah’ inazidi kung’aa ambapo Ijumaa iliyopita mrembo mwenye asili ya Kiarabu ‘shombeshombe’ aliwazidi kete mabaunsa wa msanii huyo na kumvaa mzimamzima.
Mambo ya uchaguzi! Ama kweli nyota ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Baba Tiffah’ inazidi kung’aa ambapo Ijumaa iliyopita mrembo mwenye asili ya Kiarabu ‘shombeshombe’ aliwazidi kete mabaunsa wa msanii huyo na kumvaa mzimamzima.
…Akitaka kupiga naye picha.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilijiri wakati Diamond
akishuka jukwaani baada ya kuangusha onesho la kusindikiza kampeni za
mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe
Joseph Magufuli kwenye Viwanja vya Jangwani, Dar.
Awali, wakati Diamond akikamua jukwaani, mrembo huyo alionekana
kukunwa vilivyo na makamuzi yaliyokuwa yakifanywa na Baba Tiffah ambapo
alisikika akimpigia mayowe, ‘Diamooond…I looove youuu… I neeed
youuu…Diamond kiiis me now…”
Akiwa katika hali hiyo, mdada huyo hakuna aliyemjali, kila mtu alimuona
ni shabiki wa kawaida kabla ya kuzua kizaazaa cha kumganda Diamond.
…Akizi kumng’ang’ania.
Baada ya muda Baba Tiffah alimaliza kufanya shoo na kushuka jukwaani
lakini kabla hajashuka vizuri mdada huyo alimvaa mzimamzima na
kumkumbatia huku akitaka waachwe wawili.
Kitendo hicho kiliwaamsha mabaunsa waliokuwa wakimlinda mwanamuziki
huyo ambao walianza kupambana na mrembo huyo aliyeonekana kuwazidi nguvu
na kumtia kwapani Diamond.
Alipoona ameshindwa kabisa, mdada huyo aliishia kuwanung’unikia
mabaunsa hao huku akiondoka kwa huruma akigeuka nyuma kumwangalia
Diamond kama alimuona.
Note: Only a member of this blog may post a comment.