Mwandishi Wetu
DUNIANI kuna mambo!
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja
wa Mataifa iliyopo Upanga jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita
alinaswa live ofisini kwake akiwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mzazi
wa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, kisa kikitajwa ni maandalizi ya
kuivunja amri ya sita ya Mungu, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Tukio hilo la kufedhehesha,
lilishuhudiwa na makamanda wa Global Publishers Kitengo Maalum cha
Operasheni Fichua Maovu (OFM) ambapo pia watu wengine kadhaa walijionea
kioja hicho cha mwaka.
Awali, Kamanda wa OFM akiwa kazini,
alipokea simu kutoka kwa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, akimfahamisha
juu ya hali isiyo ya kawaida kwenye ofisi za mwalimu huyo zilizopo
ndani ya geti la shule, kwani aliwaona askari polisi wakihaha kama
wanaotaka kuzuia uhalifu.
“Jamani OFM, njooni hapa Shule ya Msingi
Umoja wa Mataifa. Kama kuna ishu, naona askari wapo na pia ndani kwa
mwalimu mkuu kama kuna ishu. Sijui ni nini!” kilisema chanzo hicho.Mara
moja, kamanda huyo alifanya mawasiliano na wenzake waliokuwa ‘fildi’ na
kuwafahamisha kuhusu ishu hiyo. Wakitumia pikipiki zao ‘zinazopaa’,
makamanda hao walifika eneo la tukio dakika chache baadaye na kukuta
mambo ndiyo kwanza yanaanza.
OFM walijitambulisha kwa askari
waliokuwa eneo hilo na kuomba kwanza kupata picha kadhaa za kumbukumbu
kabla ya maelezo, ndipo ndani ofisini, walimuona mwalimu huyo akiwa na
taharuki huku akionekana kurekebisha vizuri suruali yake. Mbele yake
alikuwepo mwanamke aliyejiziba uso kwa kutumia kiganja cha mkono mmoja.
SIKILIZA UTETEZI
Alipotakiwa kutoa maelezo ya kitu
kilichokuwa kinaendelea ndani ya ofisi yake, mwalimu huyo alisema
mwanamke aliye mbele yake alikuwa akitaka kumbaka, kwani aliingia
ofisini humo na kuanza kujichekeshachekesha hovyo.
“Mkamateni mzazi huyo, anataka kunibaka. Kaja hapa, akaanza kujisemeshasemesha na kunifungua suruali yangu. Wakati namshangaa ndiyo nyinyi mnaingia,” alisema mkuu huyo huku akiichukua simu yake na kuonekana kama anayefuta kitu.
“Mkamateni mzazi huyo, anataka kunibaka. Kaja hapa, akaanza kujisemeshasemesha na kunifungua suruali yangu. Wakati namshangaa ndiyo nyinyi mnaingia,” alisema mkuu huyo huku akiichukua simu yake na kuonekana kama anayefuta kitu.
MWALIMU AWAKALISHA CHINI OFM, ASKARI
Hata hivyo, muda mchache baadaye,
mwalimu huyo aliwaomba askari na makamanda wa OFM kukaa chini na
kuyamaliza mambo hayo ili yasifike mbali.
“Jamani nyinyi ni wanaume wenzangu, mimi naomba tukae chini tuyamalize haya mambo hapahapa.”
OFM na askari hao walikataa mazungumzo hayo kwa vile kitendo cha mzazi huyo kukutwa ofisini muda huo ni chenye maswali mengi huku majibu yakiwa kiduchu.
OFM na askari hao walikataa mazungumzo hayo kwa vile kitendo cha mzazi huyo kukutwa ofisini muda huo ni chenye maswali mengi huku majibu yakiwa kiduchu.
MZAZI WA MWANAFUNZI ANENA
Akizungumza eneo la tukio, mzazi huyo
(jina kibindoni), alisema kwamba alikuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka
kwa mwalimu huyo, akimtaka kimapenzi, jambo ambalo mara zote alikuwa
akilikataa.“Huwa ananitaka, amekuwa akisema eti nikimfanikishia suala
lake atahakikisha mwanangu anasoma vizuri. Sasa mimi hadi nimechoka.
Wakati mwingine nilimdanganya nimesafiri. Siku moja nilifika hapa
almanusura afanikishe kama siyo mlango wa ofisi kugongwa.”
USHUHUDA MZITO
Mwanamke huyo alisema siku hiyo alifika
ofisini hapo baada ya kumuita, akimweleza kuwa alihitaji kuzungumza naye
juu ya maendeleo ya mtoto wake. Hapo alipinga madai ya mwalimu huyo
kuwa, alitaka kumbaka.
“Aaa! Kwa hili hawezi kukataa. Hata
tukienda kwenye kampuni ya simu ninayotumia, tukaomba watutolee karatasi
za kumbukumbu za nyuma (printout) simu ambazo tulikuwa tunapigiana
utaona kwamba, alikuwa na mawasiliano na mimi ya muda mrefu sana. Kwa
hilo asikatae, mimi sikutaka kumbaka ila yeye ndiyo alilazimisha penzi
hapa ofisini.”
Wakati mwanamke huyo akitoa ushuhuda huo, mwalimu huyo alikuwa akisikiliza kwa umakini huku akiendelea kusisitiza utetezi wake.
Wakati mwanamke huyo akitoa ushuhuda huo, mwalimu huyo alikuwa akisikiliza kwa umakini huku akiendelea kusisitiza utetezi wake.
MWALIMU APIGWA PINGU, OFM YAONDOKA
Baada ya hapo, OFM iliondoka ofisini
hapo wakati mwalimu huyo akipigwa pingu. Na kwa mujibu wa askari,
walikuwa wakienda kwenye kituo cha polisi kilicho karibu na eneo la
tukio.

Note: Only a member of this blog may post a comment.