Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Maximillian Lyimo.
Kama kandiliyetu.com tulivyowaahidi mapema leo asubuhi kuwa tutawaletea taarifa kamili kuhusu suala hili. Hii hapa tumekuwekea mdau...endelea!
Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania
Labour Party (TLP), Maximillian Lyimo ameshindwa kupiga kura leo katika
Kituo cha Njia Panda Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro baada ya
kukosekana taarifa zake kituoni hapo.
Lyimo aliyejiandikishia mkoani Dar es
Salaam, jana alienda kufunga kampeni zake Jimbo la Vunjo na kulala huko,
asubuhi ya leo alienda kituo cha Njia Panda jimboni humo ili akapige
kura.
Baada ya kufika kituoni hapo akiwa na
kitambulisho chake cha kupigia kura, alizuiwa baada ya kukosekana fomu
namba 19 ambayo kisheria inamuwezesha mgombea urais kupiga kura ya
kumchagua rais kwenye kituo chochote hivyo akakoswa fursa ya kupiga
kura.
Note: Only a member of this blog may post a comment.