Akiongea hivi punde kabla ya kuanza kutangaza matokeo mengine ya majimbo 54, Jaji Lubuva amekanusha taarifa zilizotolewa jana na viongozi wa Ukawa na kutolea ufafanuzi matokeo ya nafasi ya urais yanayopokelewa na kutangazwa na Tume hiyo.
Hivi ndivyo alivyoeleza:
"Moja ni upotoshaji unandelea sasa hivi kwamba Tume ya Uchaguzi, matokeo tunayosoma hapa yamechakachuliwa kuhusu wagombea wa urais.
"Hiyo sio kweli hata kidogo, ningependa kutumia nafasi hii kupitia ninyi waandishi wa habari kuelewesha wananchi kwamba wasipotoshwe.
“Nilishawahi kusema kwamba tunachofanya sisi hapa ni kusoma na tumeshahakiki yale ambayo yametokea katika majimbo, hayo ndiyo yaliyokuwa yamehakikiwa wakiwemo mawakala wa vyama mbalimbali.
Updates:
Lowassa anategemea kuongea tena na vyombo vya habari muda wowote mchana huu.
Endelea kufuatilia hapa kandiliyetu.com kwa updates zote muhimu za uchaguzi mkuu na matukio mbalimbali kama bado hauja-like page yetu ya facebook bonyeza hapa
Note: Only a member of this blog may post a comment.