Ijumaa: Ukiwa nyumbani na mwandani wako unapendelea kuvaa mavazi ya aina gani?
Malaika: Hahaa! Hayo ni mambo ya siri kidogo ila ni lazima nivae kimitego zaidi japo siwezi kusema navaaje.
Ijumaa: Ukishakuwa staa, ni ngumu sana kudumu kwenye uhusiano wa kimapenzi? Wewe unafanyaje ili kulinda penzi lako?
Malaika: Kikubwa ni
uaminifu na kujiheshimu, siyo wote tuna tabia chafu. Mimi nampenda
mpenzi wangu na siwezi kumpa nafasi kidudu mtu mwingine.
Ijumaa: Umefanya kazi na Chegge na ikadaiwa kuwa unatembea naye, ya kweli hayo?
Malaika: (Kicheko) sijawahi kuwa na hisia naye za mapenzi sababu Chegge namheshimu kama kaka yangu, ni maneno tu ya watu.
Ijumaa: Mastaa wengi wanapenda kuolewa kwa dau kubwa, wewe unapenda mahari yako iwe kiasi gani?
Malaika: Mimi
nimesha-chumbiwa ila hakutoa pesa bali kwa mila za kwetu za Kihaya kuna
vitu alitakiwa kuwapa wazazi na sikupiga hesabu kujua ni kiasi gani japo
ni vitu vingi vya thamani.
Ijumaa: Hivi leo Diamond Platnumz akikutokea na kutaka uzibe nafasi ya Zari utakubali?
Malaika: Hahaa sijajua, kwanza sijui warembo wanampendea nini ila mimi itakuwa ngumu kwani nimeshapendwa.
Ijumaa: Kutokana na
mvuto wako naamini wasanii wengi wenye majina wanakutaka kimapenzi,
unatumia njia gani kuwatosa ili wasikufitini kwenye muziki?
Malaika: Wanaponitokea huwa nawajibu kistaarabu tu kuwa nina mtu wangu na mara nyingi wananielewa.
Ijumaa: Kwa nini unapenda kuvaa vinguo vya kihasara wakati una mpenzi wako, huoni unawatega wanaume?
Malaika: Unajua mimi ni msanii kwa hiyo wakati mwingine nikiamua kuvaa kisanii watu wasinifikirie tofauti.
Ijumaa: Sehemu gani ya mwili wako unaipenda zaidi?
Malaika: Mwili wangu wote naupenda ila zaidi napenda miguu yangu.
Ijumaa: Kuna madai kuwa uliwahi kunasa mimba ukaichoropoa, unalizungumziaje hilo?
Malaika: Mimi sijawahi kutoa mimba na haitotokea, nikipata nitazaa sababu umri unaruhusu.
Ijumaa: Ulishawahi kuombwa rushwa ya ngono katika shughuli zako za kimuziki?
Malaika: Nashukuru sijawahi kukutwa na hilo janga la rushwa ya ngono na kama sijawahi mpaka leo sidhani kama itatokea.

Note: Only a member of this blog may post a comment.