MTABIRI maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein amesema chama cha siasa kati ya vyama viwili vikubwa nchini kitakachoshindwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wake.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum jana, Maalim
Hassan alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) vina wakati mgumu na vinashikwa kinyota kutokana na
wagombea wake kutofautiana.
“Kwa kawaida maji huzima moto lakini pia maji yakizidi, moto
huzimika, hii maana yake ni kwamba chama ambacho mgombea wake ana nyota
asili ya maji kikishinda, basi kile cha mgombea ambaye asili yake ni
maji kitakufa na moto ukizidi unaweza kukausha maji, hivyo kiutabiri
chama kitakachoshindwa kitakufa moja kwa moja au kufifia sana,”
alitahadharisha.
Chadema mwenyekiti wake ni Freeman Mbowe wakati CCM mwenyekiti wake ni Rais Jakaya Kikwete.
Uchaguzi mkuu nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kwamba matokeo ya urais
yatatangazwa ndani ya saa 72.

Note: Only a member of this blog may post a comment.