UNYAMA! Zikiwa
zimebaki siku 10 ili kupiga kura Oktoba 25, mwaka huu katika uchaguzi
mkuu, mgombea wa Udiwani Viti Maalum wilayani Butiama, Mara kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyetajwa kwa jina moja la
Upendo (39), anadai kutekwa na kundi la vijana wapatao 105 kisha kubakwa
na kuachwa katika hali mbaya
ILIKUWA SAA 11:30 JIONI
ILIKUWA SAA 11:30 JIONI
Tukio hilo la kinyama na kikatili
lilijiri Oktoba 7, mwaka huu, saa 11:30 jioni katika Kijiji cha Butuguri
wilayani Butiama ambapo mgombea huyo alikumbwa na mkasa huo baada ya
gari la mgombea ubunge wa Jimbo la Butiama kupitia Chadema, Yusufu Khazi
alilokuwa akisafiria kushambuliwa na kuvunjwa vioo na taa.
Kwa mujibu wa mashuhuda, gari hilo aina
ya Toyota Land Cruiser lenye nambari za usajili T 973 AEV lililokuwa
likiendeshwa na Masembo Paulo liliwabeba baadhi ya viongozi na wanachama
wa Chadema wakitokea kwenye mkutano wa kampeni za ubunge katika Kijiji
cha Sirorisimba ambapo mgombea wao wa ubunge yeye aliondoka na helikopta
‘chopa’
UVAMIZI
UVAMIZI
Ilidaiwa kwamba, gari hilo lilipofika
Butuguri ndipo likavamiwa na vijana hao ambao walirusha mawe na kuvunja
vioo, taa na kuwajeruhi watu tisa waliokuwa ndani ya gari hilo kabla ya
kumfanyia unyama mgombea huyo.
AOKOTWA HOI
AOKOTWA HOI
Ilielezwa kwamba, baada ya kumfanyia
unyama huo, jamaa hao walimuacha akiwa hoi ndipo akaokotwa na wasamaria
wema ambao walimkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa ajili
ya matibabu.
Akifafanua zaidi juu ya tukio hilo,
Florah Tumaini Ryana, mgombea ubunge wa Viti Maalum katika jimbo hilo
kupitia Chadema ambaye alikuwa ndani ya gari hilo na kunusurika baada ya
kutoroka kwa kukimbia, alieleza kwamba, anahisi vijana hao waliandaliwa
mahususi kwa ajili ya tukio hilo.
WALIOJERUHIWA WAFUNGULIWA MASHTAKA
WALIOJERUHIWA WAFUNGULIWA MASHTAKA
Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya
kawaida, inadaiwa kuwa majeruhi tisa walijikuta wakifunguliwa mashtaka
na viongozi wa chama kimoja cha upinzani kuhusiana na tukio hilo hali
iliyozua maswali miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.
Kesi hiyo yenye namba BUT/IR/830/2015 –SHAMBULIO ilifunguliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Butiama.
Katika jalada la kesi hiyo, watu hao
tisa wanatuhumiwa kuvamia kambi hiyo wakiwa na mapanga kwa lengo la
kuwawekea vijana hao sumu kwenye chakula.
POLISI WATHIBITISHA
POLISI WATHIBITISHA
Habari kutoka ndani ya kituo hicho cha
polisi zilieleza kwamba, waliojeruhiwa na kufunguliwa mashtaka kituoni
hapo ni John Simba Mzuzu (Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Butiama),
Pendo Juma (Diwani Viti Maalum Kata ya Sirorisimba) na Yasinta Hassan
(Diwani Viti Maalum Kata ya Kukirango).
Wengine ni Semi Jumanne (Mwanachama wa
Chadema), Edson Kanza (Mwanachama wa Chadema), Sospeter Mruta (Katibu
Baraza la Vijana wa Chadema Wilaya ya Butiama), Masemba Paulo na
Siliakusi Rashid.
Kwa upande wao polisi wilayani Butiama
walithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililoripotiwa katika Kituo cha
Polisi cha Butiama na kwamba wanaendelea na uchunguzi zaidi.
ASIMULIA MKASA MZIMA
ASIMULIA MKASA MZIMA
Kwa upande wake mgombea huyo, akiwa na maumivu makali katika kituo hicho cha polisi, alilisimulia Amani mkasa
mzima kwamba, alishangaa walipofika kijijini hapo kuona kundi la vijana
hao waliokuwa na silaha za jadi waliwavamia kisha kuwateka na kuanza
kuwashushia kipigo.
“Walikuwa vijana kama 105 hivi, walituvamia kisha wakatuteka lakini wenzangu walifanikiwa kukimbia.
“Walinishika na kuanza kunibaka na walipoona nimezimia ndipo wakakimbia.
“Ukweli wameniachia majeraha na maumivu
makali yasiyosimulika. Nawaomba watu wa haki za binadamu wanisaidie ili
sheria itende hali yake kwa sababu huu ni unyanyasaji wa kijinsia,”
alisimulia Pendo nje ya kituo cha polisi huku akitokwa machozi.
MKUU WA WILAYA ANENA
MKUU WA WILAYA ANENA
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya
ya Butiama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya, Annarose Nyamubhi alikiri kutokea kwa tukio hilo.
“Hilo tukio lipo lakini siwezi kulizungumzia zaidi kwa sababu lipo mikononi mwa polisi,” alisema Annarose.
KAMANDA WA POLISI
KAMANDA WA POLISI
Gazeti hili lilipomtafuta Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Rorya, ACP Philip Kalangi ili kuthibitisha tukio
hilo alisema yupo nje ya mkoa ila atalifuatilia.
Note: Only a member of this blog may post a comment.