Mama wa aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
NA GLADNESS MALLYA
MAMA wa aliyekuwa staa wa filamu Bongo,
Steven Kanumba, Flora Mtegoa amedai kwamba mama wa msanii Elizabeth
Michael ‘Lulu’, Lucresa Kalugira amemtukana matusi mazito
yaliyomsababishia presha na vidonda vya tumbo.
Mama wa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresa Kalugira.
Akizungumza na gazeti hili hivi
karibuni, mama Kanumba alisema wiki mbili zilizopita mama Lulu alimpigia
simu usiku wa manane na kuanza kumporomoshea matusi na kumtaka aache
kumfuatilia na mwanaye.
“Kweli hayo matusi yameniumiza, mpaka
sasa ninaumwa kwani presha inapanda kila nikikumbuka na vidonda vya
tumbo hali inayonifanya kila siku niwe ni mtu wa kwenda hospitali tu.
“Inaniuma sana kwani siku hiyo
alinitukana matusi ya nguoni, ilikuwa usiku na nahisi alikuwa kalewa,
nilipoamka siku iliyofuata nilimtafuta Lulu kwenye simu na kumweleza
lakini alirudi upande wa mama yake na kuniambia kama nina uwezo
nikashtaki popote.
“Nawashukuru Global Publishers kwa kuona
habari kwenye moja ya magazeti yenu kwamba kesi itaanza hivi karibuni,
imenipa faraja sana kwani nilikuwa nafikiria kwamba inawezekana hiyo
kesi imesahaulika,” alisema mama Kanumba.
Baada ya kupata malalamiko hayo, gazeti hili lilimtafuta mama Lulu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza sina namba ya huyo mama na tangu
nimetoka kwenye msiba wa mama yangu sijawasiliana naye, sisi ni watu
wazima sasa sijui hata tunagombea nini maana tungekuwa wasichana
ningesema labda tunagombea bwana. Anasema nilimtukana, alinirekodi au
anazumngumza tu vitu ambavyo havina ushahidi?”
Note: Only a member of this blog may post a comment.