Mwandishi wetu
WAGOMBEA wawili vinara katika uchaguzi mkuu ujao, John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Edward Ngoyai Lowassa wa Chadema, anayewakilisha umoja wa vyama vinavyounda Ukawa, sasa A silaha zao za mwisho ikiwa ni takriban wiki tatu kabla ya tukio hilo kubwa, Ijumaa linaripoti.
Duru za kisiasa kutoka kambi zote mbili zinasema, huu ni wakati wa
kubadili gia baada ya karibu mwezi mzima wa kujitangaza na kuomba kura
kulikofanywa na wagombea wote katika miji na maeneo mbalimbali nchini.
“Ukisikia lala salama ndiyo hii, zile silaha zilizokuwa zimefichwa sasa zitaibuliwa. Kuna mafaili ya hawa jamaa wa Ukawa yalikuwa yamewekwa pembeni ili kusubiri muda, naona umeshafika na sasa wapiga kura ndiyo watapewa uozo ili wasije kupoteza kura kwa ajili ya maendeleo yao,” alisema kigogo mmoja wa CCM aliyetaka jina lake lifichwe na kuongeza kuwa helikopta tano zipo tayari kusambaza sababu za chama chao kupewa kura na Watanzania.
Lakini wakati chama tawala kikijitapa kufukunyua makombora hayo, wenzao wa Ukawa wamesema mkakati wao ni kuhakikisha wanagusa kila ardhi yenye watu hapa nchini, ili kumwaga sumu kuhakikisha CCM haipigiwi kura.
“Siku zilizobaki tutazitumia kikamilifu, tumejipanga kimkakati kuhakikisha tunafika kila sehemu kwa muda muafaka, wananchi wamechoka wanahitaji mabadiliko na hivyo wanapaswa kupewa,” alitamba mjumbe mmoja wa kamati ya kampeni ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa vile siyo msemaji.
WAGOMBEA wawili vinara katika uchaguzi mkuu ujao, John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Edward Ngoyai Lowassa wa Chadema, anayewakilisha umoja wa vyama vinavyounda Ukawa, sasa A silaha zao za mwisho ikiwa ni takriban wiki tatu kabla ya tukio hilo kubwa, Ijumaa linaripoti.
Mgombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, Edward Ngoyai Lowassa wa Chadema.
“Ukisikia lala salama ndiyo hii, zile silaha zilizokuwa zimefichwa sasa zitaibuliwa. Kuna mafaili ya hawa jamaa wa Ukawa yalikuwa yamewekwa pembeni ili kusubiri muda, naona umeshafika na sasa wapiga kura ndiyo watapewa uozo ili wasije kupoteza kura kwa ajili ya maendeleo yao,” alisema kigogo mmoja wa CCM aliyetaka jina lake lifichwe na kuongeza kuwa helikopta tano zipo tayari kusambaza sababu za chama chao kupewa kura na Watanzania.
Lakini wakati chama tawala kikijitapa kufukunyua makombora hayo, wenzao wa Ukawa wamesema mkakati wao ni kuhakikisha wanagusa kila ardhi yenye watu hapa nchini, ili kumwaga sumu kuhakikisha CCM haipigiwi kura.
“Siku zilizobaki tutazitumia kikamilifu, tumejipanga kimkakati kuhakikisha tunafika kila sehemu kwa muda muafaka, wananchi wamechoka wanahitaji mabadiliko na hivyo wanapaswa kupewa,” alitamba mjumbe mmoja wa kamati ya kampeni ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa vile siyo msemaji.

Note: Only a member of this blog may post a comment.