Juma
Said Nyosso, beki na nahodha wa kikosi cha Mbeya City amefungiwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujihusisha na masuala ya
soka kwa miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili za kitanznia
kwa kosa la kumdhalilisha John Bocco wa Azam FC
Baada
ya TFF kumpiga kufuli mchezaji Juma Nyosso kujihusisha na masuala ya
soka, mchezaji huyo ameibuka na kuzungumza kwa mara ya kwanza tangu
aanze kutuhumiwa kumdhalilisha nahodha wa Azam FC John Bocco.
Nyosso
amesema uongozi wa klabu yake ulimwambia asizungumze chochote kuhusu
tukio hilo hadi pale atakapoitwa na TFF au uamuzi wa TFF utakapotoka.
Mara baada ya TFF kutoa adhabu kwa mchezaji huyo, mtandao huu uliamua
kumtafuta Nyosso na kufanya nae mazunumzo kutaka kujua amechuliaje
adhabu aliyopewa na TFF.
Hapa chini utapta majibu yote ya maswali yako kwa Nyosso kuhusiana na tukio zima lilivyotokea na adhabu aliyopewa na TFF.
Shaffihdauda.com: Baada
ya kupewa adhabu na TFF ya kufungiwa kucheza soka kwa miaka miwili
pamoja na faini ya shilingi milioni mbili, wewe unazungumziaje adhabu
hiyo ukilinganisha na kosa lenyewe?
Juma Nyosso: Mimi
nadhani hao viongozi walionihukumu mimi, walifanya haraka sana bila
kufanya utafiti wa umakini zaidi, mimi nadhani nimeonewa kwasababu ya
utashi wa watu lakini wakifatilia ushahidi zaidi kwasababu video ipo,
wangefatilia vizuri ili waje watoe hukumu sasa wameshatoa hukumu na
video inajidhihirisha.
Naomba
wafatilie ile mechi yote kuna mambo mengi yalikuwa yanatokea kwenye ile
mechi mpaka wakafikia wao kuhisi labda mimi nimefanya kile kitendo.
Mimi ni mtu mzima siwezi kurudia kitendo ambacho klabu yangu na TFF
ilishanihukumu siwezi kufanya vile hata siku moja.
Ndio
maana mimi nimekaa kimya muda mrefu kusikiliza itakuwaje na klabu
ikaniambia nisiongee na mtu yoyote tusubiri tuone itakuwaje. Mwisho wa
siku nikasikia nimefungiwa miaka miwili, unamfungia mtu miaka miwili
bila ushahidi uliokamilika nadhani kama walikurupuka au walitumia jazba.
Shaffihdauda.com: Baada ya TFF kutangaza adhau ya kukufungia kwa miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili, wewe adhabu hii uliipokeaje?
Juma Nyosso: Nimeumia
sana kwasababu mimi maisha yangu ni mpira halafu leo unaniambia
umenifungia miaka miwili na faini milioni mbili halafu ni kitu ambacho
mimi najua sikukifanya yani nimeumia sana ndio maana watu wengi walikuwa
wananipigia lakini mimi nilikuwa sitaki kuongea.
Kwasababu
viongozi wangu baada ya kufatilia ile video imeonekana kila kitu, ndio
maana mimi nimeruhusiwa kuongea. Angalia Bocco alivyokuwa akinifanyia
rafu za waziwazi lakini mwamuzi alikuwa hafanyi chochote, kwavile mimi
najulikana Nyosso tambia zangu za huko nyuma wanachukulia kwa utashi wao
wanakuja kunihukumu miaka miwili.
Shaffihdauda.com: Ukiangalia
ile video inaonekana kulikuwa na majibizano kati yako na baadhi ya
wachezaji wa Azam, kitu gani kilikuwa kinaendelea?
Juma Nyosso: Pale
yalikuwa majibizano tu ya uwanjani kwamba, cheza mpira basi ikatokea
hivyo. Mwisho wa siku naoneshwa picha lakini viongozi wakaniambia nikae
kimya kwanza. Wamefatilia wakaniambia sasa naweza kuweka wazi.
Shaffihdauda.com: Adhabu imeshatoka sasa nini kinafata sasahivi kuanzia wewe mpaka timu yako ya Mbeya City kuhusiana na adhabu uliyopewa na TFF.
Juma Nyosso: Nadhani
klabu yangu itafatilia hili suala kama ni kukata rufaa na kwavile kuna
chama cha wachezaji SPUTANZA, watalivalia njuga hili suala ili kufatilia
haki za mchezaji, haiwezekani unifungie miaka miwili wakati mpira ndio
kazi yangu unategemea miaka miwili mimi nikae nyumbani tu.
Shaffihdauda.com: Kabla
ya tukio ambalo limepelekea wewe kufungiwa, kulikuwa na matukio mengine
ambayo wewe ulifanyiwa katika mchezo huo dhidi ya Azam?
Juma Nyosso: Matukio
mengi sana ndio maana nasema video inajidhihirisha, wakae kama kamati
ya nidhamu kama ndio bodi ya ligi waangalie video yote matukio
niliyokuwa nafanyiwa mimi halafu watajiridhisha kwenye hiyo hukumu yao.


Note: Only a member of this blog may post a comment.