Chama cha soka England (FA) kimempa kocha wa Chelsea Jose Mourinho adhabu kutokana
na utovu wa nidhamu ambapo anatakiwa kulipa faini ya dola 77,000 ambazo
kibongobongo ni zaidi ya milioni 160 pamoja na kufungiwa mechi
moja huku FA wakiangalia mwenendo wake.
Meneja huyu wa Chelsea alimshambulia kwa maneno mwamuzi Robert Madley aliyechezesha mechi ya Chelsea vs Southampton iliyomalizika kwa 1- 3 na ikamfanya Mourinho akasirishwe na Refa Madley kutoipa timu yake penati na kudai Waamuzi wanaogopa kutoa uamuzi kwa timu yake.
Hii kauli ndio ikawafanya FA wamfungulie Mashitaka ya utovu wa nidhamu wakidai kauli za Mourinho zinazochochea vurugu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.