Wednesday, October 21, 2015

Anonymous

Je, Wajua Majina ya POMBE na MAGUFULI Yalipotoka? Majibu Yapo Hapa

MAGUFULI-1
Majina mawili ya Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Joseph Magufuli yana historia yake ya jinsi yalivyopatikana. Majina hayo mawili ‘Pombe’ na ‘Magufuli’ yalitokana na bibi na babu wazaa baba yake Magufuli.
Jina la ‘Pombe’ alipewa na bibi yake kwani wakati anazaliwa bibi yake alikuwa amepika pombe siku hiyo na jina la ‘Magufuli’ lilitokana na babu yake ambaye alikuwa shujaa wa kucheza ngoma za asili aliyepewa jina Magufuli kwani kila alipokuwa akicheza ngoma alikuwa anawashinda wengine hivyo kitendo hicho kilifananishwa na kufuli linavyofungwa mlangoni.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.