Sunday, October 25, 2015

Anonymous

Hii Ndio Mipango Ya Rais KIKWETE Akistaafu…(PICHAZ+SAUTI)


Rais Jakaya Mrisho Kikwete nae ameungana na Watanzania kuhakikisha anatimiza haki yake kama Raia wengine kwa kupiga Kura yake kuchagua Madiwani, Wabunge na Rais anayemrithi.

Kuna vituo vya TV vinarusha Live matangazo ya Uchaguzi Mkuu leo, Rais Kikwete kapata nafasi ya kuongea machache baada ya kupiga Kura katika Kijiji cha Msoga, nyumbani kwao Chalinze Mkoa wa Pwani.

“Nimefurahi nimepata nafasi yangu kwa kupiga Kura, naomba zoezi liwe salama… natamani Vituo vyote viwe tulivu kama hiki cha Msoga” – Rais Jakaya Kikwete.

Vipi kuhusu Ushindani wa Uchaguzi wa mwaka 2015 anavyoona? >>> “Miaka yote ushindani umekuwa mkali, nimeshiriki Uchaguzi 2005 na 2010, ulikuwa mkali tu !!“>>> Rais JK.

Mipango yake baada ya kustaafu je? >>> “Nitakuwa Rais Mstaafu, mimi ni mfugaji na ni mkulima… Baada ya hapo nitaanzisha Taasisi ya Maendeleo itakayosaidia Tanzania na Afrika na Dunia… Tarehe tano nitakuwa Rais Mstaafu.”>>> Rais Jakaya Kikwete.

Kabla ya kupita kupiga Kura, Rais JK nae alipanga foleni nyuma ya watu wengine aliowakuta Kituoni hapo.


Rais JK akiwa kwenye mahojiano na Kituo cha Azam TV baada ya kupiga Kura.

Sauti ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete hii hapa mtu wangu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.