Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima wakati wa mafunzo ya siku mbili ya waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo na wilaya na maafisa wa uchaguzi yaliyofanyika mjini Morogoro.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kwani kwa mara ya kwanza waandishi wa habari wataruhusiwa kufika katika vituo vya uchaguzi kwa lengo la kupata habari kutoka kwa wasimamizi wa uchuguzi na hata wapiga kura kuhusu namna uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 utakavyokuwa ukiendelea.
Katika hatua nyingine Kailima amesema kuwa NEC imepata taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) iliyotabiri kuwa mwezi Oktoba kutakuwa na mvua hivyo NEC imejiandaa kukabiliana na changamoto hiyo.
Hivyo amewataka wasimamizi wa uchaguzi kubaini mapema maeneo ambayo yanaweza kuingia maji na kuweka tahadhari ili kuepuka usumbufu kwa wapigakura ama uharibifu wa vifaa vya kupigia kura zikiwemo karatasi.


Note: Only a member of this blog may post a comment.