Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo October
14 ameingia kwenye headlines kwa mara nyingine tena ikiwa ni siku moja
imepita toka aingie katika rekodi ya kushinda tuzo ya kiatu cha dhahabu
mara nne.
Cristiano Ronaldo ambaye alijiunga na Real Madrid ya Hispania mwaka 2009 akitokea katika klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa dau la pound milioni 80, kiasi ambacho kiliweka rekodi ya Dunia katika masuala ya usajili amenukuliwa na vyombo vya habari akitaja umri wake wa kustaafu soka na angependa kustaafu akiwa Real Madrid.
“Ndoto
yangu ni kustaafu soka nikiwa Real Madrid kama utaweza kujitunza
vizuri unaweza kucheza soka hadi ukiwa na umri wa miaka 40, nataka
kuendelea kucheza kwa miaka mitano hadi sita Real Madrid, napanga
kuendelea kucheza kwa kiwango changu na wastani wangu huu wa ufungaji,
najisikia vizuri Madrid na nataka kuendelea kutwaa mataji hapa“>>> Ronaldo
Cristiano Ronaldo kwa sasa ana umri wa miaka 30 na mkataba na Real Madrid hadi mwaka 2018, pamoja na hayo usisahau kwamba Ronaldo siku chache zilizopita alikua akihusishwa na kutaka kurudi Man United na kujiunga na klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Note: Only a member of this blog may post a comment.