Good Morning mtu wangu leo ni Alhamisi 22 October 2015, na kama kawaida lazima asubuhi ianze na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM. Kama zilikupita na hukuzisikia zote unaweza ukacheki na hizi nyingine hapa chini kufidia.
CHADEMA, CCM nusu kwa
nusu, Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu ukomo wa madaraka ya Rais wa
nchi… Hukumu ya kesi ya mpigakura kusimama umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura kutolewa leo na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam, Edward Lowassa ameahidi kusitisha mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ili kutumia fedha hizo kuboresha bandari ya Tanga ije kuwa na hadhi ya kushindana na bandari ya Mombasa kama tu akipewa ridhaa ya kuongoza nchi kwa awamu ya tano
Mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo Mama Anna Mghwira
amesema akipewa ridhaa ya kuongoza nchi atasimamia ukusanyaji wa kodi
ili kupunguza gharama za maisha na kupambana na umasikini, kufumua
mikataba ya gesi na utalii na kuiweka wazi kwa wananchi… Rais Jakaya Kikwete leo anategemea kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la wahadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Askofu wa jimbo Katoliki Morogoro, Askofu Mkude asema nchi haitokuwa na amani kama Uchaguzi Mkuu wa October 25 hautofuata taratibu za Uchaguzi kwa amani, adai wanaosema CCM haijafanya kitu chochote cha maana wanakosea kwani ukichunguza utagundua yapo mambo mengi mazuri yaliofanywa na chama hicho.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande asema
mwaka huu watapokea kesi nyingi za Uchaguzi kutokana na hali ya kisiasa
iliyopo sasa hivi nchini na Serikali imeagiza baa zote zinazokesha
kuuza bia zisitishe huduma hiyo saa sita usiku kwenye mkesha wa Uchaguzi Mkuu ili kuepusha fujo zozote zinazoweza kuibuka tarehe 25 October 2015.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini.


Note: Only a member of this blog may post a comment.